Na Mwandishi Wetu
Rais Samia Suluhu Hassan amepokea Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award kwenye hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo Februari 4, 2025.
Tuzo hiyo hutolewa kwa viongozi waliowezesha nchi zao kuharakisha maendeleo kuelekea kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Rais Samia amepewa Tuzo hiyo katika kipengele cha mapambano dhidi ya vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga chini ya umri wa miaka mitano.