Wapigakura wapya laki nne kuandikishwa Tanga na Pwani

Na Waandishi Wetu, Tanga na Pwani

UBORESHAJI wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika mkoani Tanga na Pwani kwa siku saba kuanzia Februari 13 hadi 19, 2025 ambapo wapiga kura wapya 431,016 wanatarajiwa kuandikishwa na zoezi hilo litakapokamilika mikoa hiyo itakuwa na wapiga kura 2,727,318.

Akifungua mkutano wa wadau mkoani Tanga, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa, Jacobs Mwambegele leo Februari 01, 2025 amesema mkoani Pwani zoezihilo litafanyika kwa mkoa mzima namkoani Tanga litajumuisha Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Hpalmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto na Muheza.

“Leo tupo hapa Tanga na wenzetu wapo mkoa wa Pwani ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwenye mikoa hii, ambapo zoezi litafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 13 Februari, 2025 na kukamilika tarehe 19 Februari, 2025 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni,” amesema Jaji Mwambegele.

Akifungua mkutano kama huo mkoani Pwani, Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk amesema tayari Tume imeshakamilisha zoezi hilo kwenyemikoa 25 na kwamba mikoa ya Lindi, Mtwara na sehemu ya Mkoa wa Ruvuma inakamilisha zoezi hilo Februari 03, 2025.

Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Dodoma, Singida, Mjini Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe, Njombe na Ruvuma.

“Mikoa miwili ya Mtwara na Lindi na sehemu ya mkoa wa Ruvuma kwenye halmashauri za Madaba, Namtumbo na Tunduru inatarajia kukamilisha zoezi hilo tarehe 03 Februari, 2025,” amesema.

Mada ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Kailima Ramadhani ambayo ameiwasilisha mkoani Tanga na ambayoimewasilishwa kwa niaba yake Mkoani Pwani na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria, Selemani Mtibora imeeleza kuwa wapiga kura wapya 431,016 wanatarajiwa kuandikishwa nazoezi hilo litakapokamilika mikoa hiyo itakuwa na wapiga kura 2,727,318 sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 2,296,302 waliopo kwenye daftarikatika mikoa hiyo.

“Idadi hii inaweza kuongezeka kwakuwa inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari mwaka 2019/20, lakini kwa sababumoja au nyingine hawakuweza kujiandikisha,” imesema sehemu ya mada hiyo.

spot_img

Latest articles

Ndejembi ataka Ewura kukagua maghala ya mafuta kuhakikisha hakuna mafuta yanayofichwa

📌Asema nchi ina usalama mkubwa wa mafuta hivyo wananchi waendelee kupata huduma muda wote 📌Timu...

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

More like this

Ndejembi ataka Ewura kukagua maghala ya mafuta kuhakikisha hakuna mafuta yanayofichwa

📌Asema nchi ina usalama mkubwa wa mafuta hivyo wananchi waendelee kupata huduma muda wote 📌Timu...

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...