WAOKOAJI WA KARIAKOO WALA CHAKULA NA RAIS

Na Mwandishi Wetu

Rais Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi Januari 30, 2025  amekula chakula cha mchana pamoja na   walioshiriki uokoaji katika jengo la ghorofa lililoporomoka Kariakoo Novemba 2024.

Katika hafla hiyo ya chakula cha mchana, Rais Samia amezungumza mambo mbalimbali, huku akimtaka Waziri wa Biashara kuangaliwa suala la wageni kufanya biashara inayofanywa na wenyeji.

“Haiwezekani mgeni akawe mmachinga, vijana wetu watafanya kazi gani, kwa hiyo waziri wa biashara simamia hilo,” amesema Rais Samia.

Aidha ameeleza kuwa kupitia  mradi wa DMDP, wamejipanga kujenga soko lingine zuri kama lilivyo la Kariakoo katika eneo la Jangwani, jijini Dar es Salaam, hivyo baadhi ya wafanya biashara watahamishwa kwenda kwenye soko hilo.

Kuhusu kuporomoka kwa jengo la Kariakoo, amesema  kumewapa somo na huenda mali zinazofichwa humo hazilipiwi kodi.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amesema Kamati maalumu iliyoundwa kuchunguza kuporomoka kwa jengo la Kariakoo na kufanya ukaguzi wa kina wa majengo yaliyopo katika eneo hilo imekamilisha kazi yake na imewasilisha taarifa itakayokabidhiwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni

spot_img

Latest articles

Afariki kwa kuchomwa kisu kisa Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu Mabishano ya  ushabiki wa  Yanga na Simba yamesababisha kifo cha mwanaume mmoja...

Simba, Yanga zaondoka nchini

Na Winfrida Mtoi Timu za Simba na Yanga leo zimeondoka nchini leo kwa ajili ya...

Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba

Na Mwandishi Wetu Yanga imeendeleza ubabe kwa Simba baada ya leo kutwaa ubingwa wa Ngao...

CRDB Foundation na GIZ wazindua mradi wa Ajira Ye2, kuzalisha zaidi ya ajira 500

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la...

More like this

Afariki kwa kuchomwa kisu kisa Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu Mabishano ya  ushabiki wa  Yanga na Simba yamesababisha kifo cha mwanaume mmoja...

Simba, Yanga zaondoka nchini

Na Winfrida Mtoi Timu za Simba na Yanga leo zimeondoka nchini leo kwa ajili ya...

Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba

Na Mwandishi Wetu Yanga imeendeleza ubabe kwa Simba baada ya leo kutwaa ubingwa wa Ngao...