Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi yaanza kazi, yakaribisha wananchi kutoa maoni

Na Winfrida Mtoi

Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi nchini, imesema tayari imeanza kazi rasmi, hivyo kutoa wito kwa wananchi kutoa maoni ya kile wanachohotaji kifanyiwe maboresho katika mfumo wa ulipaji na ukusanyaji kodi.

Akizungumza leo Oktoba, 22 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam,  Mwenyekiti wa tume hiyo, Balozi Ombeni Sefue amesema wapo tayari kushirikiana na kumsikiliza kila mdau  iwe mmoja mmoja, kupitia vyama vya kitaalamu, jumuiya za biashara na nyingine ili kupata maoni yatakayowasilishwa kwa Rais Dk. Samia Suluhu.

Balozi Sefue amesema lengo ni kuhakikisha kunakuwa na mfumo bora wa kukusanya mapato na itafanya tathimini hiyo kwa kushirikisha wananchi.

“Mtakumbuka kuwa tarehe 4 Oktoba 2024, Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alizindua rasmi Tume ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Maboresho ya Kodi.

“Kama mjuavyo Tume hii imeundwa kufuatia malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji kuhusu kero mbalimbali zinazotokana na mfumo wa kodi nchini,” ameeleza  Mwenyekiti huyo.

Amefafanua kuwa Tume hiyo imepewa miezi sita lakini machakato wa kutoa maoni utachukua kipindi kisichopungua miezi miwili kuanzia sasa, baada ya hapo watachukua mapendekezo hayo, kuyafanyia tathmini na kuyachanganua kabla ya kuwasilisha kwa Rais.

Ameeleza kuwa wameandaa namna bora ya kuratibu  ushiriki wa wananchi, wafanyabiashara, wawekezaji na taasisi za umma na binafsi, asasi za kiraia, wadau wa maendeleo na wananchi wanaishi nje ya nchi ikiwamo kufanya mikutano katika maeneo mbalimbali.

Balozi Sefue amesema lengo la Serikali imedhamiria  kufikia kiwango  cha asilimia 15 ya pato la Taifa  ifikapo mwaka 2026/27  hatua itakayoongeza  uwezo wa nchi kugharamia miradi ya maendeleo na kupunguza kiwango cha utegemezi wa mikopo na misaada.

spot_img

Latest articles

C-CEOs Forum kuwa chachu ya utekelezaji wa Dira 2050

Na Mwandishi wa OTR Arusha. Serikali imesema Mkutano wa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu...

Media Brains, KAS zawajengea uwezo waandishi kutambua habari feki, washiriki   wafunguka walivyonufaika na mafunzo

Na Winfrida Mtoi Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...

EL NIÑO YABADILI RATIBA YA MITIHANI 2026

Na Mwandishi Wet Tishio la mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya hewa ya El...

TUME YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE CHAMWINO NA UDIWANI KATA 11

Na Mwandishi Wetu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza Novemba 04, 2026 kuwa...

More like this