Rais Samia azindua kitabu cha Hayati Sokoine

Na Mwandishi Wetu

Rais  Dk. Samia Suluhu Hassan leo Septemba 30, 2024, amezindua Kitabu kuhusu Maisha na Uongozi wa Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa  Tanzania mwaka 1977 -1980 na 1983- 1984, uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC)  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Rais Samia amesema mafanikio ya uongozi wa Hayati Sokoine yalichangiwa na uaminifu kwa mamlaka yake ya uteuzi, mapenzi kwa wananchi, uadilifu na uchapakazi.

Amesema maisha ya kiongozi huyo yalikuwa na mafunzo mengi na kuacha alama katika kila jukumu alilosimamia.

“Hayati Sokoine alitekeleza wajibu wake kikamilifu kama msimamizi wa shughuli za kila siku za Serikali katika kipindi kigumu na kusimama imara katika kipindi ambacho nchi ilikumbwa na changamoto za kiuchumi, uhaba wa chakula, miundombinu duni na changamoto katika sekta za viwanda na afya,”

spot_img

Latest articles

Kuporomoka majengo: Tuseme hapana kwa majanga ya kujitakia

TANZANIA ni nchi salama sana dhidi ya majanga ya asili kama vimbunga, matetemeko ya...

Rais Samia avaa viatu vya Mwalimu G20

Rio de Janeiro, Brazil RAIS Samia Suluhu Hassan ameyataka mataifa tajiri duniani ya kundi la...

Nyerere’s Footsteps, Samia Urges G20 to Rethink Global Economic Systems

Rio de Janeiro, Brazil President Samia Suluhu Hassan has rekindled the enduring vision of Tanzania’s...

Mjerumani amrithi Gamondi

Na Winfrida Mtoi Yanga imemtangaza kocha Sead Ramovic raia wa Ujerumani kuchukua nafasi ya...

More like this