Iran yanadi fursa za uwekezaji maonesho ya Sabasaba

Na Nora Damian

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imewataka wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizoko nchini humo ili kukuza kiwango cha biashara baina ya nchi hizo.

Akizungumza leo Julai 8,2024 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Iran kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Balozi wa Iran nchini Tanzania, Hossein Alvandi Vehineh, ametaja maeneo yenye fursa za uwekezaji kuwa ni katika sekta za afya, kilimo, viwanda, teknolojia na nyingine.

“Iran na Tanzania ni marafiki na tumeendelea kuchukua hatua kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo ili kukuza biashara baina ya nchi zetu,” amesema Balozi Vehineh.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), Oscar Kisanga, amewahamasisha wanachama wa chemba hiyo kuzifanyia kazi fursa hizo.

“Huwezi kufanya jambo peke yako, mimi naamini tukiunganisha nguvu kama Watanzania kwa kushirikiana na wenzetu wa Iran nina hakika tutaweza kufanya biashara na kufikia soko la dunia,” amesema Kisanga.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Latifa Khamis, ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kushiriki katika programu mbalimbali zilizoandaliwa kwenye maonesho hayo kwa kuwa zina tija katika biashara.

“Watanzania wamejitokeza kwa wingi hasa taasisi za serikali kwa ajili ya kuzungumza nao kwa sababu wamesema wako tayari kutufundisha teknolojia mbalimbali ili nasi tuweze kuzalisha…wametengeneza chanjo ya Covid ambayo inafanya vizuri hivyo, mkutano huu utazaa matunda ili nasi tuweze kutengeneza chanjo mbalimbali,” amesema Latifa.

Katika maadhimisho hayo Iran imeonesha bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa nchini humo hasa katika sekta za afya, kilimo, viwanda, mifugo pamoja na fursa ya kusoma nchini humo.

Kampuni kubwa za Iran zimeshiriki kuonyesha chanjo za wanyama na maradhi mengine kwa lengo la kutafuta wabia ili teknolojia hiyo iweze kuletwa nchini.

spot_img

Latest articles

DC Mpogolo: viongozi wa Serikali za Mitaa ni watu muhimu Katika Usimamizi wa Huduma za Umeme

Na Tatu Mohamed VIONGOZI wa Serikali za Mitaa wametajwa kuwa watu muhimu katika kusimamia miundo...

Rais Samia aagiza Tume kuchunguza, kujua haki wanayoidai vijana

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan ameielekeza Tume...

Bado denial inasuta nafsi za wengi, hatuwezi kupona

LEO ni siku ya 23 tangu risasi ya kwanza ilipofyatuliwa na kuua vijana waliokuwa...

Watoto mapacha wajinyonga Zanzibar, kisa kazi za ndani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linachunguza tukio la kujinyonga kwa...

More like this