Dk. Biteko: Kila Mtanzania atunze na kuhifadhi mazingira

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ametoa wito kwa Idara na Vitengo vya Mazingira katika wizara na taasisi za Serikali kuendelea kutekeleza majukumu yao ya msingi yanayolenga kuleta suluhisho la athari za mazingira nchini.

Akizungumza wakati wa kuzindua Mabanda ya Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani kwa Mwaka  2024 yaliyofanyika Juni 3, 2024 jijini Dodoma, Dk. Biteko amesema kuwa Serikali imeweka Vitengo vya Mazingira ili vifanye kazi ipasavyo kwa kuwa kila shughuli ina namna yake ya kuathiri mazingira na kuzuia athari zinazo tofautiana.

“Nataka nisisitize jambo hili muhimu sana kila wizara ina Kitengo cha Mazingira ni bahati mbaya kumbe kuna wakati vitengo hivi katika wizara na taasisi vimewekwa watu ambao wanadhani ni kama hawana shughuli ya kufanya, hawatengewi bajeti na hivyo hakuna shughuli ya kufanya, kazi hii imeachwa kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pekee,” amesema Dk. Biteko.

Ameendelea “Imefika mahali ukitaka kujua kuhusu mazingira basi umuone Waziri wa Mazingira peke yake wakati kila wizara ina Kitengo cha Mazingira na wajibu wake ni kuhakikisha kwamba mazingira yanahifadhiwa hata hapa kwenye uzinduzi wa mabanda ya maonesho vitengo vya baadhi ya wizara  na taasisi havipo hapa wanadhani wana majukumu kuliko mazingira,” amesema.

Aidha, Dk. Biteko amewaeleza viongozi na watumishi wa Serikali kuwa mazingira ni kila kitu huku akitolea mfano uwepo wa nguzo za umeme, ujenzi wa miradi ya barabara na hospitali nayo ni sehemu ya mazingira kwa kuwa ina uhusiano wa moja kwa moja na mazingira kwa kuharibu au kulinda na kuwa suala la mazingira linapaswa kusemwa na watu wote Serikalini katika ngazi zote ikiwemo za wakuu wa mikoa na wilaya.

Pia, Dk. Biteko amesema kuwa kutunza mazingira si kupanda miti tu bali kulinda na kuhifadhi ni jambo muhimu na lenye gharama zaidi. Aidha, ametoa wito kwa watendaji wa wizara ambao Vitengo vyao vya Mazingira havikushiriki Maonesho hayo ya Wiki ya Mazingira vijulikane ili vielezwe namna ya kutekeleza majukumu yao.

Vilevile, Dk. Biteko ametoa rai kwa Watanzania kushiriki kwa wingi katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Mazingira kitakachofanyika Juni 5, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Isdory Mpango.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dk. Selemani Jafo amesema kuwa lengo la maonesho hayo ni kutoa fursa kwa Watanzania kutembelea mabanda 42 ya maonesho ili kupata elimu kuhusu utunzaji wa mazingira pamoja na kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu teknolojia mpya za utunzaji wa mazingira na biashara ya hewa ya ukaa.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema kuwa mkoa wake umeendelea kutekeleza maagizo na shughuli mbalimbali zinazolenga kutunza mazingira na kuwa waliweka azimio la kuhakikisha wanatenga maeneo ya kuuza hewa ya ukaa na tayari Wilaya ya Mpwapwa imefanikiwa kukidhi vigezo vilivyowekwa katika kufanya biashara hiyo ikiwa ni sehemu ya utunzaji wa mazingira.

spot_img

Latest articles

Katibu Mkuu Maji aitaka DAWASA kufunga mkanda mapambano upotevu wa maji

Na Mwandishi wetu BARAZA kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi...

Rais Samia aahidi kuunda chombo cha upelelezi kubaini wahusika wa matukio ya uhalifu Oktoba 29

Na Mwandishi Wetu RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema kitaundwa chombo maalumu cha upelelezi kitakachoshughulikia masuala...

Jaji Chande: Katiba mpya, ugumu wa maisha vilichochea ghasia za uchaguzi 2025

Na Mwandishi Wetu Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya vurugu yaliyotokea wakati na...

Tume yataja idadi waliopoteza maisha matukio ya Oktoba 29, Dar yaongoza

Na Mwandishi Wetu TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na...

More like this

Katibu Mkuu Maji aitaka DAWASA kufunga mkanda mapambano upotevu wa maji

Na Mwandishi wetu BARAZA kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi...

Rais Samia aahidi kuunda chombo cha upelelezi kubaini wahusika wa matukio ya uhalifu Oktoba 29

Na Mwandishi Wetu RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema kitaundwa chombo maalumu cha upelelezi kitakachoshughulikia masuala...

Jaji Chande: Katiba mpya, ugumu wa maisha vilichochea ghasia za uchaguzi 2025

Na Mwandishi Wetu Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya vurugu yaliyotokea wakati na...