Rais Samia kuanza ziara Uturuki, Makamba asema italeta neema

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara nchini Uturuki kwa lengo la kukuza Uhusiano wa Kidiplomasia ya Siasa, uchumi na biashara kati ya nchi hizo.

Akizungumza leo Aprili 15, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema Rais Samia anafanya ziara hiyo kufuatia mwaliko alipewa na Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan.

Waziri Makamba amesema ziara hiyo itakayoanza Aprili 17 hadi 21, mwaka huu ni kubwa na ya kihistoria kwa Tanzania.

“Uturuki ni moja nchi ipo kwenye kundi la nchi 20 tajiri duniani (G20), hivyo tunajua ziara hiyo itakuwa ya kimkakakti. Lengo lingine ni kupata mtaji na teknolojia ambao nchi ya Uturuki wanayo, kupata masoko ya bidhaa ambayo yapo nchini humo na kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwetu,” amesema Mamkamba.

Amesema tayari wameshuhudia kampuni kubwa kutoka Uturuki zikifanya shughuli mbalimbali hapa nchini hatua ambayo imekuwa ikisaidia kuchochea maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwamo za elimu, afya na maji.

Makamba amesema Rais Dk. Samia atafanya mazungumzo ya Kiserikali na Rais wa Uturuki na baadae watafanya mazungumzo ya pamoja na wajumbe wa pande zote mbili lengo likiwa ni kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano.

Amesema miaka 14 iliyopita Rais aliyekuwepo madarakani alifanya ziara nchini humo na Rais wa Uturuki alikuja nchini mwaka 2017 hivyo kuna uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.

“Tuna uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia tangu mwaka 1963 huku tukiwa tumefungua Ubalozi wetu mwaka 1979, baadae ubalozi huo ulifungwa mwaka 1984 kutokana na changamoto mbalimbali, ulifunguliwa tena mwaka 2009.

“Sisi tulikuwa na ubalozi nchini Uturuki uliofunguliwa mwaka 2017 hapo utaona kuwa uhusiano wetu ni mzuri kwa muda mrefu,” amesema Waziri Makamba.

Amesema Nchi ya Uturuki imekuwa haraka kiuchumi na ni nchi iliyopata maendeleo haraka kutokana na uhusiano na nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.

“Tunajua kuna wafanyabiashara wengi wanakwenda Uturuki kununua bidhaa na sisi tunauza huko bidhaa zetu,” amesema Waziri Makamba.

spot_img

Latest articles

Serikali yaahidi kushirikiana na wadau kuendeleza mchezo wa kuogelea

Na Winfrida Mtoi WADAU wa mchezo wakuogelea Afrika Mashariki wamekutana kujadili maendeleo ya mchezo huo,...

Ndejembi: Tanesco mmefanya mageuzi makubwa katika huduma ya umeme kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kuwa Shirika la Umeme Tanzania...

Dube awapa raha wananchi

Na Winfrida Mtoi BAO pekee lililofungwa na Prince Dube dakika ya 58, limeipa Yanga alama...

Mexico yatwaa taji la Miss Universe 2025, Ivory Coast namba tano

Na Mwandishi Wetu Mexico imeibuka mshindi wa taji la Miss Universe 2025 kupitia mrembo wake...

More like this

Serikali yaahidi kushirikiana na wadau kuendeleza mchezo wa kuogelea

Na Winfrida Mtoi WADAU wa mchezo wakuogelea Afrika Mashariki wamekutana kujadili maendeleo ya mchezo huo,...

Ndejembi: Tanesco mmefanya mageuzi makubwa katika huduma ya umeme kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kuwa Shirika la Umeme Tanzania...

Dube awapa raha wananchi

Na Winfrida Mtoi BAO pekee lililofungwa na Prince Dube dakika ya 58, limeipa Yanga alama...