Dk. Biteko azitaka TARURA, TANESCO kufikisha huduma Ngorongoro

*Aipongeza TBC kwa maboresho makubwa ya miundombinu

*Usikivu wa radio za TBC kufikia asilimia 92 Mwaka 2024/2025

*Asisitiza maamuzi sahihi uchaguzi Serikali za Mitaa

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameagiza Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuhakikisha linapeleka huduma ya umeme kwenye maeneo ya miradi ya maendeleo ili kuharahisisha huduma kwa wananchi.

Dk. Biteko amesema hayo akiwa Loliondo, wilayani Ngorongoro baada ya kuzindua minara ya kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo fm.

Amesema miradi inatekelezwa na itakuwa ya mafankio endapo Taasisi husika zitakaa pamoja na kuandaa maeneo yanayohitaji utekelezaji katika hatua mbalimbali.

“TANESCO, REA, UCSAF na TBC zikae pamoja wakati wa uandaaji wa miradi husika ili miradi iwe inatekelezeka kwa tija, ufanisi na kwa haraka,” amesema Dk. Biteko.

Pia, ameiagiza TARURA kuhakikisha huduma ya barabara zinafikika katika maeneo ilipojengwa mitambo ya redio ambayo ipo sehemu kubwa ya milimani nchini ili kuwa na miundombinu imara.

Pia, ameipongeza TBC kwa maboresho makubwa ya miundombinu ya utangazaji, maboresho ya studio, mitambo na vifaa vya kisasa, ubora wa maudhui pamoja na ubunifu katika kuwahabarisha Watanzania.

“Mimi nafuatilia habari za TBC nafahamu chaneli ya TBC mahsusi kwa ajili kutangaza utalii (Safari Chaneli), redio ya vijana ya Bongo FM na televisheni ya vijana ya TBC2. TBC imekuwa na kampeni maalum kama vile: 27 ya Kijani kupitia Jambo Tanzania, Elimu kwa Umma kuhusu Tume ya Haki Jinai, vipindi vya kimkakati vyenye lengo la kukuza uzalendo (Mizani, jioni njema, jamvi la machweo na Lulu za Kiswahili),” amesema Dk. Biteko.

Katika hatua nyingine, Dk. Biteko amewataka wananchi ambao mitambo hiyo imezinduliwa katika wilaya za Ngorongoro, Arusha, Uvinza Kigoma, Makete – Njombe na Kyela Mbeya, kuhakikisha wanaitunza mitambo hiyo kwa maslahi ya wananchi wote.

“Nimetaarifiwa kuwa usikivu wa redio za TBC katika kipindi cha miaka mitatu (2020/2021 – 2022/2023) ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umeongezeka kutoka asilimia 74 (2020/2021) hadi kufikia asilimia 85 (2022/2023) na utafikia asilimia 92 baada ya kukamilika miradi inayoendelea kwa Mwaka huu wa Fedha 2023/2024,” amesema Dk. Biteko.

Kuhusu uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa amewasihi watanzania kufanya maamuzi sahihi kwa kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo kwani Wananchi wanachotaka ni maendeleo na sio siasa.

“Tujitahidi kusikiliza vizuri sera za wagombea watakaoamua kuwania na tuamue kwa utulivu na kwa kumshirikisha Mwenye Mungu ili lengo kuu la kuwa na viongozi lifikiwe,” ameongeza Dk. Biteko.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema TBC inaendelea kuboresha miundombinu ya utangazaji ili kuwahabarisha Watanzania.

Aidha, amewataka Watanzania kusimama na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Rais amegusa maisha ya Watanzania kwa kuleta fedha na kujenga ncjo, kuboresha miundombinu mbalimbali hapa nchini.

spot_img

Latest articles

DAWASA KUFANYA MATENGENEZO KINGA, MAJI KUKATIKA KWA SAA 12

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)...

OTR kuongeza kasi ya mageuzi ili kukuza tija ya uwekezaji

Na Mwandishi Wetu Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) imejizatiti kuongeza kasi ya mageuzi ya...

Mikono ya Kitanzania, Gesi ya Tanzania: Bomba la Gesi kutoka Kisemvule–Mbagala Linaenda Kasi

Kampuni ya Rashal Energies Limited, chini ya Afisa Mtendaji Mkuu Farhiya Warsame, yajenga bomba...

SAPP kufungua Fursa kwa Tanzania Kuwa Kitovu cha Biashara ya Umeme Kusini mwa Afrika

📌Nchi 18 Zakutana Zanzibar kujadili usalama wa nishati ya umeme kusini mwa Afrika 📌Kuuza au...

More like this

DAWASA KUFANYA MATENGENEZO KINGA, MAJI KUKATIKA KWA SAA 12

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)...

OTR kuongeza kasi ya mageuzi ili kukuza tija ya uwekezaji

Na Mwandishi Wetu Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) imejizatiti kuongeza kasi ya mageuzi ya...

Mikono ya Kitanzania, Gesi ya Tanzania: Bomba la Gesi kutoka Kisemvule–Mbagala Linaenda Kasi

Kampuni ya Rashal Energies Limited, chini ya Afisa Mtendaji Mkuu Farhiya Warsame, yajenga bomba...