Polisi wawasaka walioua, kukata nyeti za marehemu

Polisi mkoani Mwanza wanawasaka wahusika wa mauaji ya Masanja Kefa (32) mkazi wa Kijiji cha Mwagig’hi, Kata ya Nkalalo wilayani kwimba, kukata sehemu zake za siri kisha kutoweka nazo. Tukio hilo linalohusishwa na imani za ushirikina, Februari 12, 2024.

Ofisa Polisi Jamii Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhani Sarige amesema wakati polisi wakiedelea na uchunguzi wa tukio hilo, wakazi wa Kijiji cha Mwagig’hi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa ambazo zitawezesha waliotenda uhalifu huo kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

ACP Sarige amesema hayo Februari 26, 2024 akiwa ameambatana na baadhi ya maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wakati wakitoa elimu ya Polisi Jamii kwa wakazi wa kijiji hicho.

“Tumewaletea Polisi Kata lengo likiwa ni kuimarisha ulinzi shirikishi lakini mmempokea kwa tukio hili la kikatili, si vyema kuendekeza vitendo hivi vya kishirikiana, tuhakikishe tunashirikiana katika ulinzi shirikishi ili kukomesha vitendo hivi,”anasema Sarige na kuongeza:

“Tunajua watu hawa mnawafahamu na wengine wanaweza kuwa ni ndugu zetu, hivyo tusiwafiche wahalifu hawa kwani leo kwake, kesho kwako. Kama kafanya hivyo kwa huyo, umemtunza kesho atakufanyia wewe.”

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamewapongeza polisi kwa kuimarisha ushirikiano na kuwa karibu hasa wakati huu ambao wamesema ni mgumu, na wameahidi kutoa ushirikiano ili kuwapata wahalifu waliohusika na tukio.

spot_img

Latest articles

Sekta ya Viwanda na Biashara yazidi kutoa fursa kwa vijana

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amesema sekta ya viwanda...

Polisi yachunguza tukio la kuchoma moto magari msibani

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema linachunguza tukio la kuchoma moto na...

Taifa Stars yakabidhiwa bendera tayari kwa AFCON 2025

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, ameiaga na...

CRDB yashirikiana na Kids’ Holiday Festival kukuza elimu ya fedha kwa watoto

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imeingia makubaliano ya ushirikiano na Kids’ Holiday Festival...

More like this