Rais Samia amlilia Lowassa

RAIS SAMIA AMLILIA LOWASSA

RAIS Sami Suluhu Hassan ametuma salaam za rambirambi kwa familia ya Hayati Edward Lowassa, ambaye amefariki leo katika Hospitali ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.

“Mheshimiwa Lowassa ameitumikia nchi yetu katika nafasi mbalimbali kwa zaidi ya miaka 35, akianzia ushiriki wake katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbunge, Waziri katika wizara mbalimbali na Waziri Mkuu,” anasema Rais Samia kwenye mtandao wake wa X na kuongeza: “Tumempoteza kiongozi mahiri, aliyejituma na kujitoa kwa nchi yetu. Natoa pole kwa mjane, Mama Regina Lowassa, watoto (Mheshimiwa Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa na wadogo zako), ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mzito.”

Rais amesema katika mawasiliano yake na familia, amewaeleza kuwa: “Kama taifa tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu, na kamwe wasiache kumtegemea Mwenyezi Mungu na kutafakari neno lake, hasa Kitabu cha Ayubu 1:21.”

spot_img

Latest articles

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

Uwanja wa KMC wafungiwa

Na Mwandishi Wetu  SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limeufungia uwanja wa KMC, uliopo Mwenge, jijini...

More like this