102 wafutiwa matokeo ya kidato cha nne

Na Esther Mnyika

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA),  limefuta matokeo  ya watahiniwa 102 wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2023 kutokana na udanganyifu na   waliondika lugha ya matusi kwenye karatasi za majibu.

Matokeo ya  ya kitado cha nne yametangazwa  leo Januari 25, 2024 jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa  NECTA, Dk.Said Mohamed.

Amesema  kati  hao waliofutiwa matokeo, watano  waliondika matusi, wakati  matokeo ya wanafunzi 376 yakizuiwa kutokana na kupata  matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani.

Dk.Mohamed amesema watahiniwa walioshindwa kufanya mtihani huo mwaka jana  wamepewa fursa ya kufanya masomo ambayo hawakuyafanya kwa sababu ya ugonjwa  kwa mujibu wa Kifungu cha 32(1) cha Kanuni za Mitihani.

Dk. Mohammed amesema jumla ya watahiniwa 572,359 walisajiliwa kufanya mtihani huo Novemba mwaka jana ambapo 484,823 sawa na asilimia 87.65wamefaulu.

Amesema wasichana waliofaulu ni 257,892,   wavulana wakiwa 226,931, huku masomo ya lugha ikiwamo kichina yakifanya vizuri zaidi.

Amesema  wanafunzi waliofaulu masomo ya kiswahili  asilimia 96.80 na kichina ni 91.36

“Kati ya watahiniwa 471,427 waliofaulu, wasichana ni 250,147 sawa na asilimia 88.11 na wavulana ni 221,280 sawa na asilimia 90.81. Hivyo, wavulana wamefaulu vizuri zaidi kuliko wasichana,” amesema.

Hata hivyo NECTA imezipongeza  Kamati za Uendeshaji Mitihani za Mikoa na Halmashauri, Manispaa na Jiji, wakuu wa shule, wasimamizi na wasahihishaji wa mtihani huo  kwa kazi nzuri ya kutekeleza jukumu la uendeshaji  mtihani huo.

spot_img

Latest articles

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

Viongozi wa dini waendelea kihimiza amani uchaguzi mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam VIONGOZI wa dini nchini wameendelea kuhimiza umuhimu wa kudumisha...

Ujumbe wa viongozi wa dini kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025 katika Kongamano la Kamati ya Amani Kitaifa Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu Askofu Mkuu Wapo Mission, Dk. Sylvester Gamanywa “Mungu ambaye tunamwakilisha ndiye anayweka watawala...

Watumishi wa umma waaswa kushiriki Uchaguzi wa Oktoba 29

Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) imetoa wito kwa watumishi wote...

More like this