Walimu watakiwa kutimiza wajibu kwa kufanya kazi kwa bidii

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Walimu wa shule za msingi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wametakiwa kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuinua kiwango cha taaluma katika halmashauri hiyo.

Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mussa Ally, akizungumza wakati wa hafla ya Siku ya Elimu Kata ya Ukonga.

Wito huo umetolewa Oktoba 13,2023 na Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mussa Ally ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, wakati wa hafla ya Siku ya Elimu Kata ya Ukonga.

Amesema Serikali inawathamini walimu kwa kushughulikia stahiki zao mbalimbali kama vile kulipa madeni hivyo ni wajibu wao kufanya kazi na maarifa huku wakitembea kwa kujivuna kwamba Serikali inawajali.

“Walimu ni jeshi kubwa, tuendelee kuwa wamoja kwa sababu sisi ndio walezi wa taifa, tuendelee kuitumikia Serikali kwa haki na wajibu,” amesema Mwalimu Ally.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mzambarauni walioratibu hafla hiyo Maria Liyombo, amesema siku hiyo ina lengo la kuwakutanisha walimu ili kuimarisha uhusiano na kuinua taaluma katika Kata ya Ukonga.

“Tunawaunganisha walimu na kuwajengea ari ya kufanya kazi na kuwakumbusha wajibu wao, tunataka kuifanya Kata ya Ukonga kuwa ya mfano katika taaluma Jiji la Dar es Salaam,” amesema Mwalimu Liyombo.

Kata ya Ukonga ina shule 15
za msingi na awali 15 na kati ya hizo nane ni za Serikali na saba za watu binafsi.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this