Warning: Array to string conversion in /home/themedia/domains/themediabrains.com/public_html/wp-includes/shortcodes.php on line 434
Array

Wawekezaji wakumbushwa kuendelea kuchangia katika miradi ya maendeleo

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Jenista Mhagam, ametoa rai kwa wawekezaji wa mbalimbali katika jimbo la Peramiho kuendelea Kufanya uwekezaji wenye tija kwa wananchi, kwa Halmashauri na kwa Taifa.

Waziri Mhagama ametoa rai hiyo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Muhukuru katika ziara yake ya kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Songea Julai 12, 2023.

“Tunataka wawekezaji wajue wana wajibu wa kuchangia shughuli za maendeleo kwenye vijiji vinavozunguka maeneo uwekezaji,” amesisitiza.

Makaa ya mawe yamekuwa bidhaa muhimu na adhimu, uwekezaji umeendelea kukua na masoko yameongezeka, wawekezaji waangalie ajira zile zinazosaidia kuendesha miradi yao ili kutoa kipaombele katika maeneo ya vijjiji vilivyozunguka mradi, alisema Waziri Mhagama.

“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi nzuri ya kuvutia Wawekezaji Mbalimbali, Wawekezaji wa shamba la miwa, wawekezaji wa makaa ya mawe na wawekezaji wa umeme wa maji, naomba kila Mwekezaji aliyeomba ardhi ya uwekezaji atumie kama alivyoomba,” amesema Mhagama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea, Menas Komba amesema uwekezaji wa makaa ya mawe kuna mpango kabambe ambao umelenga kupata asilimia moja ya kila awamu ya mauzo.

“Tuendele kushirikiana na wawekezaji wanaokuja kuwekeza ili waendelee kutusaidia na Halmashauri itasimamia kupata haki za wananchi,” amesema Komba

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea, Mwalimu Neema Maghembe amesema wawekezaji wote waliowekeza katika Halmashauri ya Songea wamefuata taratibu zote za uwekezaji.

“Tunawawekezaji wa kutosha, wengine wanaendelea na kazi za tafiti mbalimbali na wengine wako katika hatua ya kuanza uchimbaji wa makaa ya mawe,” amesema Mwalimu Maghembe.

spot_img

Latest articles

Mavazi ya kitamaduni kivutio kingine AFCON 2025

Na Winfrida Mtoi SHAMRASHAMRA kuelekea Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2025), zimezidi kupamba moto, hasa baada...

Livembe: Mchakato wa Uchaguzi ulikuwa wa haki na halali

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Hamis Livembe, amesema mchakato wa...

Sekta ya Viwanda na Biashara yazidi kutoa fursa kwa vijana

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amesema sekta ya viwanda...

Polisi yachunguza tukio la kuchoma moto magari msibani

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema linachunguza tukio la kuchoma moto na...

More like this

Mavazi ya kitamaduni kivutio kingine AFCON 2025

Na Winfrida Mtoi SHAMRASHAMRA kuelekea Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2025), zimezidi kupamba moto, hasa baada...

Livembe: Mchakato wa Uchaguzi ulikuwa wa haki na halali

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Hamis Livembe, amesema mchakato wa...

Sekta ya Viwanda na Biashara yazidi kutoa fursa kwa vijana

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amesema sekta ya viwanda...