Warning: Array to string conversion in /home/themedia/domains/themediabrains.com/public_html/wp-includes/shortcodes.php on line 434
Array

Viongozi wa Serikali za vijiji wahimizwa kuweka uwazi walengwa wa TASAF

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema ni jukumu la Watendaji wa Serikali za Vijiji kuwatambua wananchi ambao wanastahili kuingizwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia mikutano ya vijiji ili kuwepo na uwazi pamoja na kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi ambao wana vigezo vya kuingizwa.             

Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kata ya Masaki, Kijiji cha Kisanga Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Kikwete amesema kuwa, kuna baadhi ya wananchi ambao wanastahili kuingizwa kwenye mradi wa TASAF wenye sifa na vigezo lakini kutokana na kutoitishwa mikutano ya kijiji hupelekea baadhi yao kukosa nafasi ya kuingizwa kwenye mradi huo, hivyo amewataka viongozi hao kuendesha mikutano ya mara kwa mara ili kuondoa malalamiko ambayo yanaweza kutokea.

Aidha, Kikwete amesisitiza wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa akijitahidi kuboresha maisha ya wananchi wake kwa maendeleo ya Taifa la Tanzania.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete anaendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao pamoja na kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF.

spot_img

Latest articles

Viongozi Chadema washinda shauri la kuidharau Mahakama

Na Mwandishi Wetu Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imetupilia mbali shauri la maombi...

Ridhiwani:Niko tayari kuhojiwa kuhusu tuhuma za Lake Oil

Na Mwandishi Wetu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na...

Ndejembi: Ufanisi wa Tanesco katika utekelezaji na Usimamizi wa miradi umeleta mfumo madhubuti wa Nishati

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema kuwa Shirika la Umeme...

Maboresho ya mitambo ya kufua umeme Mtera yaimarisha uzalishaji umeme

Na Mwandishi Wetu, Mtera NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, Novemba 26, 2025, alitembelea na...

More like this